MAISHA YA NAIBU WA RAIS ALIYENG'ATULIWA MAMLAKANI YAKO HATARINI
Katiba ya Kenya inalenga kulinda haki za kimsingi za raia wake na kuimarisha ulinzi wa haki za kibinadamu katika Nyanja zote za kijamii, kiuchumi Na kisiasa. Hivyo basi ni jambo la busara Rigathi Gashagua kupeleka malalamishi yake kuwa maisha yake yako hatarini kwa idara hiyo. Aidha, mashtaka yake yatategemea iwapo ana ushahidi wa kutosha ili idara hiyo ichukue hatua na kuanza uchunguzi mara moja.
Tatizo kubwa Kwa Gashagua ni iwapo viongozi wakuu katika serikali kuu wanahusika. Hivyo basi wana ushawishi mkubwa ndani ya serikali na katika Nyanja tofauti ikiwemo idara hii ya upelelezi wa jinai na wanaweza kusababisha kesi hiyo kutupiliwa mbali. Vile vile kuna uwezekano pia idara hiyo kutotilia maanani malalamishi yake ikizingatiwa kwamba aling’atuliwa mamlaka hivi karibuni na anaweza kuwa anandaa makosa dhidi ya serikali kama njia mojawapo ya kupinga uamuzi wa serikali wa kumng’atua mamlakani.
Hatua hii itaonyesha uwazi na uwajibikaji katika serikali. Hii Ni njia mojawapo ya kulinda sheria na kuhakikisha kuwa watu wanawajibika kwa matendo yao ikiwemo viongozi. Hatua hiyo kama njia ya kuimarisha mfumo wa sheria nchini Kenya.


Comments
Post a Comment