MAUAJI YA KIHOLELA YA WANAWAKE NCHINI KENYA
Kulingana na kamanda mkuu wa polisi Douglas Kanja kumekuwa na ongozeko kubwa la mauaji ya watu mpaka 339 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kufuatia visa hivi, Kamanda wa polisi pia amehimiza wakenya kuripoti tukio lolote la kutiliwa shaka kwenye vituo za polisi.Aidha, asimilia kubwa ya mauaji haya, yanahusisha wanawake.Vitendo hivi vinatikisa usalama wa mtoto msichana nchini Kenya na kuwaacha wengi na maswali chungunzima.
Mnamo Januari tarehe 27 wanawake walitokea mtaani kuhamasisha umma kuhusu mauaji ya kiholela ya wanawake. Haya yalikua maandamano makubwa kuweza kuandaliwa nchini Kenya kutokana na ukatili wa kijinsia. Maandamano yaliandaliwa kufuatia mauaji ya yaliyotingiza vyombo vya habari na kuwashangaza wengi. Angalu wanawake 14 waliangamia mwezi wa Januari peke yake kufuatia mauaji ya kiholela. Kati ya visa hivyo ni ikiwemo mauaji ya mwanaharakati maarufu Scarlet Wahu na mwanafunzi wa chuo Kikuu Rita Waeni aliyeuawa kikatili na kukatwa viuongo vya mwili.
Hivi karibuni Kenya imekumbwa na mauaji mengine ya kikatili yaliyohusisha mama na watoto wasichana wawili mtaani Eastleigh kaunti ya Nairobi. Jambo la kusikitisha ni kuwa wote Kati ya waliouliwa walikua wanawake. Kulingana na utafiti wa shirika la Data Hub Africa asilimia kubwa ya mauaji yaliyofanyika kufikia mwaka huu wa elfu mbili ishirini na nne ni kutokana na ukatili wa kijinsia. Hii ni kwasababu katika visa vingi muuaji alikua anafahamiana na muadhirika. Shirika hili la Data Hub pia limebaini kuwa kutoka 2016 angalau wanawake mia tano wameuawa kikatili licha ya juhudi za nchi ya Kenya kupambana na janga hili.
Swali ni je Kenya itachukua hatua gani kupambana na mauaji kutokana na ukatili wa kijinsia?Ama iwapo itajiunga na nchi ya Costa Rica ambayo ni nchi ya kwanza kupitisha mauaji ya wanawake kama uhalifu unaotambulika kisheria ili kukabiliana kikamilifu na janga hili


Comments
Post a Comment